Utafiti mpya kutoka kampuni za kura ya maoni Newspoll na The Guardian, umedokeza kuwa baadhi yawapiga kura bado hawaja fanya maamuzi ila watu wengi zaidi wana nia yakupiga kura ya la badala ya ndio.
Kiongozi wa NSW Chris Minns amesema mpango wa jimbo lake wa nishati mbadala, hauendi vizuri na sasa ata ingia katika mazungumzo na kampuni ya nishati ya Origin Energy, kuongeza maisha ya kituo kikubwa zaidi cha nishati ya makaa ya mawe nchini Australia. Ripoti huru iliyo tolewa leo jumanne 5 Septemba, imependekeza kuzingatia kuendelea kutumia kituo cha umeme kinacho milikiwa na Origin katika eneo la Central Coast jimboni humo, ziadi ya muda ulio pangwa kufungwa katika mwaka wa 2025.
Rais wa Kenya William Ruto, amewaomba wajumbe wanaohudhuria mkutano wa kilele wa hali ya hewa barani Afrika kutumia mkutano huo kusaidia kutoa mapendekezo chanya ya Afrika yatakayopelekwa kwenye mkutano wa hali ya hewa duniani COP28 utakaofanyika Dubai mwezi Novemba. Mkutano huo ambao unafanyika mjini Nairobi, unawajumuisha wakuu wa nchi, watunga sera, viongozi wa serikali, watoa maamuzi, wataalam wa mabadiliko ya hali ya hewa, mashirika ya kimataifa na mashirika ya kiraia, na sekta binafsi.
Waziri wa mambo ya ndani Peter Kazadi amesema polisi wamewakamata kanali Mike Mikombe aliyeongoza kikosi cha ulinzi wa rais mjini Goma na Luteni Kanali Donatien Bawili aliyeongoza kikosi cha jeshi la Congo katika mji huo ambako machafuko yalitokea.
Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika ya Kati ECCAS imeamua kusimamisha unachama wa Gabon kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 30 yaliyomuondoa madarakani rais Ali Bongo. Jumuiya ya ECCAS imetoa taarifa hiyo baada ya kikao chake kilichofanyika jana Jumatatu katika mji mkuu wa nchi jirani ya Guinea ya Ikweta, Malabo.