Manowari ya nyuklia ya Marekani imewasili katika jimbo la Magharibi Australia, kupiga doria ya kawaida katika kanda hiyo wakati Marekani ina ongeza juhudi yakuthibitisha dhamira yake kwa ukanda wa Pasifiki.
Katika taarifa zakusikitisha, watoto watano pamoja na baba yao wame uawa kupitia moto ulio choma nyumba moja katika kisiwa cha Russell jimboni Queensland. Mwanamke mwenye umri wa miaka 28 anaye amiwa kuwa mama ya watoto hao alipona, na amepokea matibabu ya kupumua moshi ila hakupata majeraha kimwili. Mwanamke mwingine mwenye miaka 21 aliye dhaniwa kuwa ndani ya nyumba hiyo moto huo ulipo anza naye pia alifanikiwa kujiokoa.
Serikali ya Ufaransa ilisema Jumamosi itaunga mkono juhudi za kurejesha uongozi wa kiraia nchini Niger kufuatia mapinduzi ya kijeshi, siku moja baada ya jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS kusema kuwa una mpango wa kuingilia kijeshi.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilisema Ijumaa kuwa imelazimika kufunga ofisi yake nchini Uganda na kwamba itasitisha rasmi shughuli zake nchini humo Jumamosi.
Baraza la mawaziri la Ethiopia limetangaza hali ya dharura katika mkoa wa Amhara, baada ya mamlaka kuomba msaada kufuatia kuongezeka kwa mapambano kati ya vikosi vya kieneo na jeshi la serikali. Ofisi ya waziri mkuu imetangaza hali hiyo mapema leo baada ya viongozi wa kieneo kusema kwamba mafisa wa usalama wameshindwa kudhibiti hali, ingawa bunge linahitaji kuidhinisha hatua hiyo.