Taarifa ya habari 6 Aprili 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Waziri Mkuu Scott Morrison amesema tangazo la New Zealand kuhusu usafiri wa watu kati ya Australia na New Zealand bila mahitaji ya karantini, ni hatua muhimu kwa nchi zote mbili.


Kwa upande wake Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern, amesema wasafiri wanastahili jiandaa kwa usumbufu kwa mipango yao ya usafiri, patakapo kuwa mlipuko wa COVID-19.

Zaidi ya idadi yamashirika 20 nchini yame omba waziri mpya Linda Reynolds, asitishe mipango ya mageuzi kwa mfumo wa dhamana yakitaifa ya ulemavu maarufu kwa ufupi kama[[NDIS]]. Makundi hayo yana ogopa mageuzi kwa tathmini huru yata ondoa uadilifu wa mfumo wa N-D-I-S pamoja nakudhoufisha uwezo wa washiriki kuweza kufanya uamuzi nakudhibiti maisha yao.

Mzozo kati ya Kenya na Uingereza umeendelea kutokota baada ya serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki kutangaza masharti mapya kwa abiria wanaotoka au kupitia Uingereza. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara Mambo ya Nje ya Kenya, masharti hayo yataanza kutekelezwa kuanzia Aprili 9, 2021, ambayo ni siku ya Ijumaa.

 


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service