Taarifa ya Habari 6 Disemba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri mkuu atupilia mbali madai kuwa haja toa taarifa, kwa washirika wake kwa mpango wakupunguza bei ya nishati.


Upinzani wa mseto wa taifa ume ishtumu sera yakiuchumi ya serikali ya Albanese, baada ya ongezeko ya kiwango cha riba kutoka kwa benki ya hifadhi. Benki ya hifadhi imeongeza kiwango cha riba cha hela taslim nchini AUstralia, kwa alama 25, na sasa kiwango hicho ni 3.10% ambacho ni kiwango cha juu zaidi tangu 2012.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken ameambia rais wa Rwanda Paul Kagame kuacha kutoa msaada kwa kundi la waasi la M23 linalopigana na serikali ya Kinshasa, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema kwamba waziri Blinken amefanya mazungumzo ya simu na rais wa Rwanda Paul Kagame na kuzungumzia umuhimu wa kuwepo amani na utulivu mashariki mwa DRC. Blinken amesema kwamba Marekani inaunga mkono juhudi za amani zinazofanywa na jumuiya ya Afrika mashariki na mpatanishi wa umoja wa Afrika, ambaye ni rais wa Angola Joao Lourenco.

Viongozi wakuu wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC wanafanya mazungumzo tangu leo asubuhi kujadili hatma ya rais Cyril Ramaphosa anayekabiliwa na shinikizo la kisiasa linaloweza kumwondoa madarakani. Rais Ramaphosa mwenyewe ni miongoni mwa wale wanaoshiriki majadiliano hayo yanayofanyika siku moja kabla ya bunge kupiga kura inayoweza kuanzisha mchakato wa kumtoa mamlakani. Kiongozi huyo anaandamwa na kiwingu cha madai ya kukiuka katiba baada ya jopo maalum la uchunguzi kuchapisha ripoti iliyomtuhumu kuficha taarifa za wizi wa maelfu ya dola uliotokea kwenye shamba lake binafsi.







Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service