Waziri wa shirikisho wa afya na huduma yawazee Greg Hunt ametetea sifa za waziri mkuu, hii ni baada ya ujumbe mfupi wa simu uliovuja kutoka kwa naibu waziri mkuu Barnaby Joyce, ulio sema kwamba waziri mkuu Scott Morrison ni kigeugeu na mwongo. Bw Joyce ameomba msamaha kwa ujumbe wake uliotumwa Machi mwaka jana, na aliomba kujiuzulu ila Bw Morrison haku kubali ombi hilo.
Kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika kimeanza Jumamosi mjini Addis Ababa, Ethiopia na kauli mbiu yam waka huu “Kuimarisha Uwepo wa Lishe na Usalama wa Chakula katika bara la Afrika. Wamekutana ili kuimarisha mifumo ya uzalishaji chakula, mifumo ya afya na ustawi wa jamii kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya binadamu, kijamii na kiuchumi.” Viongozi kutoka kote barani humo walikusanyika kujadili masuala yanayoliathiri bara hilo; hasa janga la Corona na ukosefu wa usalama.
Mvulana mwenye umri wa miaka mitano aliyeanguka kwenye kisima kirefu kwa siku nne amefariki, licha ya juhudi za kumuokoa. Taarifa ya ufalme wa Morocco ilitangaza kifo mara ya baada ya mvulana huyo kuondolewa kwenye shimo. Juhudi za kumuokoa mvulana huyo, anayeitwa Rayan, zilifuatiliwa kote nchini, huku mamia ya watu wakikusanyika kwenye shimo na maelfu zaidi wakifuatilia shuguli ya uokozi ,kupitia mtandao.