Wa Australia kukaza mikanda zaidi baada ya benki ya hifadhi kuongeza kiwango cha riba tena na, kampuni za usafiri wa anga zakabiliwa kwa shinikizo yakuboresha huduma kwa wateja wao.
Rwanda yaiomba Malawi kuisaidia kuwakamata wahusika wa mauaji ya kimbari, Rais Ruto awaonya wabunge wa mrengo wa Kenya Kwanza dhidi yakupinga muswada wa fedha na maandamano ya vurugu yaendelea kushuhudiwa Senegal baada ya mmoja wa viongozi wa upinzani kupewa hukumu ya miaka mbili gerezani.
Timu ya raga ya NSW yapigwa jeki kupitia matokea chanya kwa vipimo vya nyota wao kabla ya mechi ya pili ya State of origin, sherehe zaendelea Central Coast baada ya ubingwa wao katika fainali ya ligi kuu na Australia kuwa na mwalimu wa kwanza katika historia ya ligi kuu ya Uingereza.