Taarifa ya Habari 6 Novemba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya shirikisho imekubali kukutana na vikundi vya biashara katikati, kwa baadhi ya sehemu tata za muswada wamahusiano ya viwanda.


Wakaaji katika jamii za NSW zilizo athiriwa na mafuriko, zimeanza kwa utaratibu kufanya tathmini ya uharibifu ulio sababishwa na maji ya mafuriko katika maeneo ya ndani ya miji yao. Mto Lachlan ambao uko Forbes katika eneo la kati magharibi ya jimbo hilo, ulifika kilele cha takriban urefu wa mita 10.7 Jumamosi, kiwango hicho kikiwa chini kidogo ya rekodi iliyowekwa 1952.

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekua na mazungumzo na rais Joao Lourenco mjini Luanda juu ya kuongezeka kwa uhasama na mapigano mashariki ya Congo. Mvutano kati ya nchi hizo mbili ulianza kua mbaya mapema mwishoni mwa mwaka jana 2021 pale kundi la M23 lenya kuongozwa na watutsi wa Congo kuamua kuchukua silaha na kuanza kupambana na jeshi la taifa la Congo FRDC.

Maelfu ya abiria wa shirika ndege la Kenya Airways wamekwama baada ya marubani wa shirika hilo kuanza mgomo siku ya Jumamosi asubuhi ulolazimisha kufutwa kwa mamia ya safari. Serikali ilijaribu kuwahimiza marubani wa moja wapi ya shirika kuu la ndege barani Afrika kutofanya mgomo wao, lakini inaonekana juhudi hazikufanikiwa.

Vyombo vya habari nchini Tanzania vimeripoti kuwa ndege ya kampuni ya Precision Air imepata ajali na kuanguka katika ziwa Victoria ilipokuwa ikielekea katika uwanja wa ndege wa Bukoba. Bado haijabainishwa idadi ya abiria waliokuwa katika ndege hiyo ama iwapo kuna watu waliopoteza maisha. Ripoti hizo zinaonesha picha za ndege hiyo ikiwa zaidi imezama ndani ya ziwa hilo na kusema juhudi za uokoaji zimeanza.Mashuhuda wanasema ajali hii imetokana na ndege hiyo kupata hitilafu ilipokuwa ikitua.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service