Taarifa ya Habari 6 Oktoba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Wataalam wamesema Australia inahitaji makumi yama elfu ya nyumba za ziada zakukodi, wakati viwango vya nyumba zakukodi vinarejea katika viwango vya chini katika rekodi hali ambayo imeongeza kodi sana.


Tovuti yamatangazo ya nyumba zaku kodi Domain imepata kuwa upatikanaji wa nyumba zakukodi uliporomoka katika robo ya Septemba hadi kiwango cha 0.8%, hicho kikiwa kiwango cha chini zaidi tangu Machi takwimu hizo ziki ashiriwa na ongezeko la uhamiaji.
Viwango vya nyumba zakukodi katika miji yote ya Australia vinakaribia, au viko kwenye rekodi za chini, wakati soko za upangaji tata zikiwa mjini Perth na Adelaide. Miji ya Brisbane na Darwin inafuata kwa karibu, wakati miji mingine mikuu nchini imesalia kwa 1.6%

Mwanasheria wa haki za binadam David Manne amesema anatumai mageuzi mpaya ya serikali, yata punguza pakubwa mkwamo wa maombi ya viza za ulinzi za waomba hifadhi.
Serikali imesema baadhi ya watu wana wasilisha inacho ita madai ya uongo ya hifadhi, wame weza kubaki nchini kwa hadi miaka 11 kabla ya kesi zao kukamilishwa. Imetangazwa kuwa mpango wenye thamani ya $160 milioni, waku shughulikia maombi katika hali ambayo inasema ni haraka zaidi na yenye usawa.

Wakaaji wa maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki Victoria, wanaendelea kujiandaa kukabiliana na mafuriko wakati maji yana endelea kuongezeka siku chache baada ya kanda hiyo kukabiliwa kwa moto wa vichaka. Onyo la mafuriko limetolewa kwa eneo la Port of Sale [[October 5]], wakati wakaazi wame elezwa na huduma za dharura waondoke na waelekee sehemu za juu, na zaidi ya onyo za 'tazama na chukua hatua' zimewekwa kwa jamii za karibu ya Wangaratta.

Rais wa Kenya William Ruto Jumatano alifanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri, kuongeza wizara mpya, na kuwateua maafisa wapya kuchukua nyadhifa mbalimbali serikalini. Mawaziri 8 ni kati ya waliohamishiwa kwa wizara nyingine huku majukumu ya Waziri Mkuu Musalia Mudavadi yakiongezwa, na idara moja kuondolewa kutoka kwa afisi yake. Rais Ruto pia aliwateua makatibu wakuu kadhaa, mabalozi na manaibu wao, huku akiwahamisha wengine kuhudumu katika wizara au balozi mbalimbali.

Mahakama nchini Burundi imemnyima dhamana waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Alain-Guillaume Bunyoni, ambaye ameshtakiwa kwa shutuma za kuhujumu usalama wa taifa na kumtusi rais, vyanzo karibu na kesi hiyo vililiambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi. Bunyoni alikuwa waziri mkuu kuanzia katikati ya mwaka 2020 lakini aliachishwa kazi kutokana na mzozo wa ngazi ya juu wa kisiasa mwezi Septemba mwaka 2022, siku chache baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kuonya kuhusu njama ya "mapinduzi" dhidi yake.

Kiongozi wa upinzani wa Congo Moise Katumbi amewasilisha ombi lake la kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Desemba ambapo Rais Felix Tshisekedi anawania tena nafasi hiyo kwa muhula wa pili, chama chake kilisema siku ya Jumatano.
Katumbi, mfanyabiashara tajiri mkubwa na gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga wenye utajiri wa shaba, pia atashindana dhidi ya Martin Fayulu - ambaye aliibuka mshindi wa pili katika uchaguzi uliopita - na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya magonjwa ya wanawake Denis Mukwege na wengineo.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amesema siku ya Alhamisi amewekwa katika kizuizi cha nyumbani, baada ya kukamatwa na maafisa wa usalama alipokuwa akirejea nyumbani akitokea nje ya nchi. Wine, mwanamuziki maarufu aliyegeuka kuwa mwanasiasa aliyeshindana na Rais mkongwe Yoweri Museveni katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021 nchini Uganda, amekuwa akikamatwa mara nyingi.



Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service