Serikali ya shirikisho imesema mfumo wakutoa alama za ubora kwa makaazi ya huduma ya wazee, unatarajiwa kutumiwa kufikia mwisho wa mwaka huu. Mfumo huu utatoa alama kwa makaazi kwa maswala tofauti ya malezi na huduma, kuruhusu familia zichague makaazi yanayo tosheleza mahitaji yao.
Watu wenye silaha wamewaua watu sita, wakiwemo W]wahindi wawili, katika jimbo la Kogi nchini Nigeria, polisi walisema Jumamosi, huku eneo hilo likikumbwa na ghasia za wanajihadi na magenge.
Wagombea urais nchini Kenya, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga na Naibu wa Rais William Ruto, Jumamosi walihutubia mikutano yao ya mwisho ya kampeni mjini Nairobi kwelekea kwa uchaguzi mkuu Jumanne wiki ijayo. Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi, Jumamosi ilikuwa siku ya mwisho kwa wagombea, vyama na miungano ya kisisasa kufanya mikutano ya kampeni kote nchini.