Serikali ita tekeleza mapendekezo yanayo salia kutoka tathmini huru, ya bodi ya watendaji wa kodi, wakati idara ya hazina itafanya tathmini ya adhabu na sheria za siri. Seneta wa chama cha Labor Deborah O'Neill, ambaye amekuwa sehemu mhimu yakufichua taarifa kuhusu uvujaji wa kodi wa kampuni ya P-w-C, amesema serikali imejibu ipaswavyo matokeo ya tathmini hiyo.
Mbunge huru Kate Chaney amewasilisha muswada kwa jina la ‘Kurejesha uaminifu’, muswada huo unalengo lakuboresha uwazi katika siasa. Muswada huo una mageuzi 13 yanayo ungwa mkono na wabunge wengine huru na vyama vidogo. Muswada huo unapendekeza mageuzi kadhaa, yanayo jumuisha kuweka wazi anaye mfadhili mgombea, taarifa ya papo hapo kwa michango yakisiasa ambayo inazidi dola elfu moja, pamoja na kupiga marufuku uongo katika kampeni zakisiasa. Muswada huo pia unapiga marufuku michango yakisiasa kutoka kile ambacho Bi Chaney ame elezea kuwa ni, sekta za madhara yakijamii kama, sigara, pombe na kamari kwa ajili yaku hakikisha maamuzi yanafanywa kwa maslahi yawa Australia. Bi Chaney ame ongezea kuwa muswada huo una piga jeki kazi ya tume yakitaifa dhidi ya ufisadi.
Waziri wa afya wa shirikisho Mark Butler amesema ana nia yakurejesha imani kwa sekta ya madawa katika jamii, wakati madawa ya bei nafuu yana wasilishwa. Kuanzia Septemba 1, mamilioni yawagonjwa wanao ishi na hali sugu za afya, wataweza pokea mara mbili madawa wanayo hitaji, kwa gharama ya hati moja. Hata hivyo, chama cha Liberal na washawishi wa maduka yamadawa wana kosoa hatua hiyo wakisema, wakaazi wa huduma za wazee pamoja nawa Australia wakongwe wata beba gharama yamaduka yamadawa.
Ila Bw Butler amesema serikali ina nia yaku wekeza hela tena, zitakazo okolewa kutoka hatua hizo pamoja na uwekezaji wa dola milioni 350 za ziada, kwa huduma za maduka ya dawa yanayo tolewa katika makaazi ya huduma yawazee. Waziri wa Afya kwa upande wake, amekosoa anacho ita kampeni ya woga kutoka chama cha Liberal na washawishi wa maduka yamadawa.
Kiongozi wa upinzani wa Senegal Ousmane Sonko, ambaye amekuwa akisusia chakula wakati akiwa gerezani kama njia ya kulalamikia mashitaka ya jinai dhidi yake, Jumapili amelazwa hospitalini, kulingana na ripoti kutoka chama chake. Sonko alipelekwa jela wiki iliyopita kabla ya kesi yake kusikilizwa, akituhumiwa kuitisha mapinduzi dhidi ya serikali miongoni mwa mashitaka mengine. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP sababu hasa ya Sonko ya kulazwa kwenye hospitali kuu mjini Dakar haijatolewa, ingawa alikuwa buheri wa afya bila kuwa na maradhi yoyote yanayojulikana kabla ya kuwekwa jela, chama chake kilichopigwa marufuku cha Patriots of Senegal kimesema. Hapo Julai 30, Sonko kupitia ukurasa wake wa Twitter ambayo sasa inafahamika kama X alisema kwamba angeanza kususia chakula. Tangazo hilo lilikuja siku moja tu kabla ya jaji wa mahakama ya Dakar kuamuru apelekwe jela. Mashitaka ya karibuni dhidi ya Sonko yamekuja wiki chache baada jaji kumpata na hatia ya kuchochea vijana na kutoa hukumu ya miaka 2 jela, hatua iliyosababisha maandamano makali kote nchini.
Maelfu ya wafuasi wa utawala wa kijeshi walimiminika kwenye uwanja wa michezo mjini Niamey katika mji mkuu, wakishangilia uamuzi wa kutosalimu amri. Niger ilifunga anga yake siku ya Jumapili hadi itakapotoa taarifa baadaye, ikielezea tishio la kuingiliwa kijeshi kutoka jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi baada ya viongozi wa mapinduzi kukataa amri ya kumrejesha madarakani rais wa nchi hiyo aliyepinduliwa. Awali, maelfu ya wafuasi wa utawala wa kijeshi walimiminika kwenye uwanja wa michezo mjini Niamey katika mji mkuu, wakishangilia uamuzi wa kutosalimu amri shinikizo kutoka nje kutimiza maagizo ifikapo Jumapili kufuatia unyakuaji madaraka wa Julai 26.
Na katika michezo:
Australia imeshinda kombe la dunia la mchezo wa pete kwa mara ya 12, katika ushindi ambao ulikuwa niwakulipiza kisasi dhidi ya Uingereza kwa vikapu 61-45. Timu ya English Roses ya Uingereza ilisababisha mtikisiko baada yakuishinda Australia, katika hatua yamakundi siku ya Alhamisi hatua ambayo ilikuwa ni ushindi wao wa kwanza dhidi ya Diamonds wa Australia. Hata hivyo Diamonds hawakuwa na huruma katika fainali hiyo iliyo chezwa jana Jumapili mjini Cape Town.
Katika soka ya kina dada, Marekani Jumapili iliondolewa kwenye kombe la dunia la Wanawake mwaka 2023 baada ya kushindwa na Sweden kupitia mikwaju ya penalti. Sweden iliishinda Marekani kwa mabao 5-4 na kufuzu kuingia kwenye robo fainali na kumzuia bingwa huyo wa mara mbili kutwaa mataji matatu ya kihistoria mfululizo. Mechi hiyo ilichezwa mjini Melbourne, Australia, iliamuliwa kwa njia ya video (VAR), huku mwamuzi Stephanie Frappart - baada ya kukagua yaliyojiri- akiona kuwa penalti ya Lina Hurtig ilivuka mstari licha ya Mlinda lango wa timu ya Marekani Alyssa Naeher kugusa mpira huo, na kuonekana kama angeokoa timu yake.