Taarifa ya Habari 7 Disemba 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Walimu wa shule za umma pamoja na walimu wakuu wame andamana kote jimboni NSW, dhidi ya mishahara midogo pamoja na kazi nyingi.


Shinikizo inaongezeka kwa Waziri Mkuu Scott Morrison achukue hatua dhidi ya mbunge George Christensen, baada ya mbunge huyo kushiriki kwenye makala mtandaoni ya nadharia ya njama potovu, ambako alihamasisha umma uandamane dhidi ya vizuizi vya UVIKO-19 vya Australia. Bw Christensen alishiriki katika makala ya InfoWars ya Mmarekani Alex Jones, ambako alihamasisha waandamanaji wajumuike nje, balozi za Australia kuandamana dhidi ya hatua dhidi ya coronavirus. Makala ya InfoWars yamepigwa marufuku kwenye Facebook na YouTube, kwa kukiuka sera za kauli za chuki, na msimamizi wa makala hayo Alex Jones, ametoa madai kadhaa ya uongo na yanayo potosha kuhusu janga hili.

Kambi ya Mtendeli, moja ya kambi tatu za Tanzania zinazohifadhi wakimbizi wa Burundi imefungwa kabisa, baada ya zaidi ya wakimbizi elfu 19 wa mwisho waliokuwa katika kambi hiyo kuhamishiwa kwenye kambi ya Nduta Jumatatu. Maafisa hao wanasema usalama utaimarishwa ikiwa zitabaki kambi mbili pekee, ile ya Nyarugusu na hiyo ya Nduta ambayo ndiyo kambi inayohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi wa Burundi. Taarifa zinaendelea kusema kwamba viongozi wanapanga pia kuwahamisha wakimbizi wote wa Burundi wanaopatikana katika kambi ya Nyarugusu na kuwapeleka kwenye kambi ya Nduta. Wakimbizi kutoka Congo ndio watabaki katika kambi ya Nyarugusu, taarifa zimeendelea kusema. Wakimbizi elfu 3 waliokuwa Mtendeli walirejea nyumbani kwa hiara hiyo tangu mwezi Julai mwaka huu.

Serikali ya Ethiopia imetangaza kuidhibiti tena miji miwili ya kimkakati ya Dessie na Kombolcha, mwezi mmoja baada ya kushikiliwa na wapiganaji wa Tigray. Hatua hiyo ni ya hivi karibuni katika mfululizo wa ushindi wa haraka katika uwanja wa vita unaotangazwa na vikosi tiifu vya waziri mkuu Abiy Ahmed. Idara ya mawasiliano ya serikali imesema katika tangazo la kupitia Twitter kwamba miji ya Dessie na Kombolcha imekombolewa na vikosi vya usalama vya pamoja, ambavyo pia vilichukua udhibiti wa miji kadhaa upande wa mashariki.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service