Taarifa ya Habari 7 Juni 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Mweka hazina wa taifa afariji familia zawa Australia zinazo kabiliana, na madhara yakiuchumi ya ongezeko ya kiwango cha riba, hali ambayo imefikisha kiwango cha hela taslim kuwa 0.85


Benki ya hifadhi imeongeza kiwango cha hela taslim kwa alama 50 leo Jumanne, ambayo ni ongezeko kubwa zaidi kuliko ilivyo tarajiwa na wachumi wakati mfumuko wa bei nao ume ongezeka. Mweka hazina wa taifa Jim Chalmers, amesema uamuzi wa hivi karibuni utaweka shinikizo kwa bajeti za familia ila, anatambua kuwa serikali inaweza saidia kuimarisha uchumi. Kwa upande wake, msemaji wa hazina katika upinzani Angus Taylor, amesema ni mhimu kusitisha matumizi ya serikali yasiyo lazima.

Wanajeshi wawili wa DRC wameuawa Jumatatu katika mapigano dhidi ya waasi wa M23 huko mashariki mwa nchi, jeshi la DRC limesema. Ni ghasia za hivi karibuni katika mzozo huo wa muda mrefu ambao uliibuwa katika wiki za hivi karibuni na kusababisha mvutano wa kidiplomasia na nchi jirani ya Rwanda. Waasi wa M23 walishambulia kwa makombora kituo cha jeshi huko Kivu Kaskazini, na kuua wanajeshi wawili na kujeruhi wengine watano. DR Congo inamshtumu jirani yake kuunga mkono kundi la M23, tuhuma ambazo Rwanda inakanusha.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anakabiliwa na uchunguzi wa makosa ya jinai baada ya taarifa iliyofichuliwa kuwa hakuweza kuripoti wizi wa takriban dola milioni 4 pesa taslimu kwenye shamba lake kaskazini mwa jimbo la Limpopo. Ramaphosa hakukanusha kwamba wizi huo ulifanyika lakini alidai kwamba aliuripoti kwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wake, ambaye hakuripoti wizi huo kwa polisi.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service