Taarifa ya Habari 7 Mei 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Zaidi ya idadi ya nyumba milioni tano nchini pamoja na biashara ndogo milioni moja, zitapata afueni ya $500 kwa bili za nishati katika bajeti ya shirikisho ya Mei 9.


Ma milioni ya watu kote duniani walitazama Mfalme Charles lll akitawazwa, kwa hisia mseto kwa siku za usoni za ufalme nchini Australia.

Kiongozi wa upinzani wa Victoria John Pesutto amesema ata unga mkono muswada waku mtimua mbunge tata kutoka chama cha Liberal. Moira Deeming anaweza ondolewa katika chama hicho kwa sababu ya utata ulio zuka alipo hudhuria, maandamano yakuwapinga watu wanao jifanya kuwa wa jinsia tofauti na yao ya asili, mjini Melbourne ambako kundi laki Nazi lilikuwa pia.

Mashambulizi ya anga yaliushambulia mji mkuu wa Sudan siku ya Jumamosi huku mapigano yakiingia wiki yake ya nne saa chache kabla ya pande zinazohasimiana kukutana nchini Saudi Arabia kwa mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Jumamosi aliwasihi viongozi wa Afrika kuzidisha juhudi zao za kuleta amani huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mahala ambako makundi yenye silaha yamekwua yakiwatisha raia kwa miongo kadhaa.

Mhubiri mwenye utata wa kanisa la Good News International lililopo kaunti ya Kilifi Malindi,Kenya na mkewe Rhoda Mackenzie pamoja na na watuhumiwa wengine 16 wamefikishwa katika mahakama ya Shanzu. Waendesha mashtaka wanaomba kumshikilia Mackenzie, ambaye alianzisha Kanisa la Good News International Church mwaka wa 2003, kwa siku nyingine 90 hadi uchunguzi utakapokamilika.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service