Taarifa ya Habari 7 Novemba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya Albanese inasema mahusiano na China, yako katika sehemu nzuri kuliko mwaka jana, wakati Waziri Mkuu Anthony Albanese ana endelea na ziara yake nchini humo.


Upinzani wa shirikisho umesema serikali ya Albanese inahitaji fany "kazi ya ziada" kukabiliana na mfumuko wa bei kabla ya utabiri wa ongezeko ya kiwango cha riba katika siku ya mashindano ya Melbourne Cup Day. Viwango havija ongezeka kwa miezi minne mfululizo ila, sasa wachumi wanatarajia bodi ya benki kuu itaongeza viwango vya riba leo kwa 0.25% hali itakayo chukua kiwango cha hela taslim kufika 4.35%.

Sheria mpya zinazo toa ulinzi katika sehemu ya kazi ime gawanywa leo, katika hatua inayo ruhusu baadhi ya vipengee ambavyo si tata vya mageuzi hayo kupitishwa mara moja. Muswada huo utaziba mapengo yanayo ruhusu waajiri kulipa kiwango kidogo cha hela, kuongeza ulinzi kwa wafanyakazi wenye mikataba mifupi, pamoja nakuruhusu wafanyakazi hao wahamie katika kazi zakudumu.

Serikali ya Afrika Kusini ilisema Jumatatu itawarejesha wanadiplomasia wake wote walioko Israel kutokana na wasiwasi wake kuhusu hali ya huko Gaza. Pretoria pia imesema nafasi ya balozi wa Israel nchini humo imekuwa “zaidi na zaidi isiyoweza kutegemewa", akimtuhumu mwanadiplomasia aliyetoa "matamshi ya dharau" kuhusu watu wanaoikosoa Israel.

Bunge la Tanzania limehitimisha mjadala wa Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2022, lakini baadhi ya wasomi na wanasiasa wameonyesha wasiwasi na kuwataka wananchi kuwashinikiza wabunge kuchukua hatua dhidi ya wanaoshutumiwa kufuja fedha za umma. Tuhuma hizo zimekuwa zikielezewa katika ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.

Mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Somalia yamepelekea zaidi ya watu 113,000 kuhama makwao, huku wengine maelfu wakiathiriwa na hali hiyo, kulingana na ofisi ya UN ya kuratibu masuala ya kibinadamu, UNOCHA. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, takriban watu 10 wamekufa kufuatia mvua hizo, wakati serikali ikitangaza hali ya dharura, Idara ya kitaifa ya dharura ya Somalia imesema kupitia ukurasa wake wa X, uliojulikana kama Twitter.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service