Uwekezaji huo uta elekezwa kwa ujenzi wa nyumba 11 zenye huduma zote ndani, kwa ajili yakuwasaidia wanao kimbia unyanyasaji wa nyumbani.
Utafiti umabaini kuwa wa Australia wanaunga mkono uwasilishaji wa vikomo vya kodi, pamoja na pendekezo kuwa wanaweza unga mkono kufunguwa kwa bunge na uchaguzi mkuu kuitishwa kwa sababu ya hoja hiyo. Hoja ya matumizi ya ziada kwa nyumba za bei nafuu, nayo ina endelea kuungwa mkono pia.
Mbunge huru Kate Chaney, amewasilisha muswada 'wakurejesha uaminifu' ambao unalengo lakuboresha uwazi katika siasa. Muswada huo una mageuzi 13 yanayo ungwa mkono na sehemu kubwa ya wabunge wengine huru na vyama vidogo. Muswada huo unapendekeza mageuzi kadhaa yanayo jumuisha kuweka wazi anaye mfadhili mgombea, taarifa za papo hapo za michango yote yakisiasa inayo zidi dola elfu moja, pamoja nakupiga marufuku uongo katika kampeni zakisiasa.
Viongozi wa Afrika Magharibi Jumatatu walipanga mkutano utakaofanyika Alhamisi kujadili hatua ya serikali ya Niger kukataa amri ya kumrejesha madarakani rais aliyeondolewa mamlakani na hivyo kuibua matumaini ya kimataifa ya kutafuta suluhu bila ya kutumia nguvu.
Watu wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi katika siku ya tano ya maandamano ya ghasia katika mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini yaliyosababishwa na mzozo wiki iliyopita kati ya madereva wa mabasi madogo na mamlaka.
Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limeitolea mwito serikali ya Tanzania kuacha kuwakandamiza wakosoaji wake baada ya mamlaka za nchi hiyo kuwakamata watu wanaopinga mkataba wa uendeshaji bandari.
Katika michezo Matildas watinga robo fainali ya kombe la dunia wakati, matarajio ya Nigeria kutinga robo fainali yagonga mwamba mjini Brisbane.