Mawakili wa ustawi wameomba malipo ya jobseeker yaongezwe kwakudumu, kabla ya mpango wakuyapunguza ulio ratibiwa 1 januari kutekelezwa. Nyongeza ya coronavirus ilikuwa $550 kila wiki mbili katika mwanzo wa janga ila, imepunguzwa hadi $250 na itapunguzwa zaidi hadi $150 kila wiki mbili kuanzia tarehe 1 Januari, iwapo muswada huo utapitishwa bungeni.
Serikali ya Somalia Jumatatu ilisimamisha utoaji wa vibali vinavyotolewa kwenye uwanja wa ndege nchini humo kwa wageni kutoka Kenya. Ofisi ya uhamiaji ya Somalia imesema kuwa hatua hiyo imepelekewa na tahadhari dhidi ya maambukizi ya Covid19. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, amri hiyo itaanza kutekelezwa Diseemba 13.
Wawakilishi wa wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania wameandika barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Guterres na Kamishna Mkuu wa umoja huo anayeshughulikia Wakimbizi Grandi kuomba makazi katika nchi nyingine. Barua hiyo imesema kuwa baadhi ya wakimbizi wananyanyaswa na kurejeshwa kwao bila kufuata utaratibu maalum ndio maana wanaomba taifa lingine liweze kuwapokea.