Taarifa ya Habari 8 Februari 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Scott Morrison ame muomba msamaha mfanyakazi wa zamani wa chama cha Liberal Brittany Higgins, kwa madai ya ubakaji dhidi yake ndani ya bunge la taifa pamoja na wanawake wengine ambao, wame umizwa kimawazo, nakunyanyasiwa ndani ya bunge la taifa.


Baada ya marudio yake ya tatu, chama tawala cha mseto kime idhinisha mageuzi machache, kwa muswada wa ubaguzi wadini pamoja na muswada wa ubaguzi wajinsia. Hiyo ilikuwa katika mkutano ulio ongezewa muda wa chama tawala, baada ya muda wa maswali na majibu bungeni mapema mchana wa leo jumanne. Serikali ya shirikisho inajaribu kupitisha muswada huo ila, mivutano ya ndani inatishia kuvuruga muswada huo kupitishwa.

Umoja wa Afrika umefunga mkutano wake wa kila mwaka Jumapili ambako viongozi wamekubaliana kusitisha mjadala juu ya uamuzi wenye utata wa Moussa Mahamat Faki Mwenyekiti wa Tume ya AU kuikubali Israel na kuaihirisha kura ambayo ingekuwa na mgawanyiko. Uamuzi wa Faki wa Julai mwaka 2021 ulisababisha upinzani kutoka kwa wanachama wenye ushawishi ikiwemo Afrika Kusini na Algeria ambazo zilisema kwamba ilionyesha kubeza taarifa za AU kuunga mkono maeneo ya Palestina.

Wahudumu wa afya kutoka mataifa 99 ulimwenguni wamekutana Jumatatu Mombasa, Kenya kujadili mtaala wa pamoja kwenye nyanja ya utabibu. Mkutano huo ambao utamalizika Jumatano ni wa kwanza wa aina yake unalenga kushughulikia mtaala wa elimu kwa wahudumu wa afya na jinsi ya kutumia teknolojia ya kisasa kuimarisha utoaji huduma kufikia viwango vya kimataifa.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service