Wanaharakati wamesema wanawake bado wanakabiliana na changamoto nyingi, katika harakati zao zakupigania usawa, pamoja na ubaguzi katika sehemu za kazi. Shirika la habari la SBS limezungumza na baadhi ya wanawake ambao wamesema, wame pitia uzoefu wakushushwa vyeo, kulazimishwa kuondoka kazini au, kazi zao kufutwa baada ya wao kupata watoto.
Ujumbe wa maafisa waandamizi wa Marekani ulikwenda nchini Venezuela Jumamosi kwa mazungumzo na wajumbe wa serikali ya Rais Nicolas Maduro kuangalia uwezekano wa kupunguza vikwazo vya Marekani dhidi ya taifa hilo ambalo ni mzalishaji mkubwa sana wa mafuta kwa mujibu wa vyanzo ambavyo vilishiriki katika mazungumzo hayo. Vyanzo vinasema mazungumzo yamekuwa yakifanyika kwa siri kwa miezi kadhaa huku utawala wa Biden ukipima njia ya kupunguza vikwazo na kushauriana kuhusu kuachiliwa kwa raia wa Marekani ambao wameshikiliwa nchini Venezuela. Lakini wanasema mazungumzo yalichukua mwelekeo wa haraka kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.
Naibu wa Rais wa Kenya, William Ruto, ambaye pia ni mgombea urais nchini humo, amesema kuna tetesi za mipango ya kukataa kumtangaza kama mshindi wa uchaguzi wa urais, baada ya zoezi kufanyika tarehe tisa mwezi Agosti mwaka huu. Hali kadhalika mwanasiasa huyo alisema kuna njama za kuizuia jumuiya ya kimataifa, kutoa msaada wa vifaa, na wa kimikakati, kwa tume ya uchaguzi ya na mipaka ya Kenya, IEBC, kujiandaa kwelekea kwa uchaguzi huo mkuu.