Watoto jimboni New South Wales watapewa mwaka mmoja wa ziada katika huduma za chekechea, kama sehemu ya mfuko wenye thamani ya dola milioni 120 ambazo zimetolewa na serikali ya jimbo hilo.
Rais mteule wa Marekani Biden na makamu wake, Kamala Harris, wametowa hotuba zao za kwanza za shukrani kufuatia ushindi wao kwenye uchaguzi uliokuwa na mchuano mkali, huku Trump akikataa kuyatambua matokeo hayo.
Rais Mteule John Magufuli Alhamisi ameapishwa kuiongoza tena Tanzania baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu nchini humo juma lililopita. Magufuli anaingia katika kipindi cha pili cha uongozi wake huku akitaka taifa hilo kuungana pamoja baada ya uchaguzi wakati upinzani nchini humo ukitangaza kutotambua ushindi wake.