Mji wa kanda wa Lismore ambao uko kaskazini New South Wales, unajiandaa kwa tukio kubwa la tatu la mafuriko mwaka huu. Jana jumatatu, eneo hilo lilipokea mililita 127 ya mvua katika muda wa masaa 19. Wakati huo huo, kiongozi wa New South Wales Dominic Perrottet, ame anza ziara yamaeneo ya kanda yaliyo athiriwa kwa mafuriko leo Jumanne.
Waziri wa uhamiaji amehamasisha mtu yeyote ambaye amepitia uzoefu wa unyanyasaji kama mfanyakazi wauhamiaji, ajitokeze na ameahidi kutumia mbinu yakutokuwa na uvumilivu kwa mtazamao huo. Tathmini mpya itaanzishwa kuchunguza madai ya vyombo katika vyombo vya habari kuhusu, unyanyasaji wa wafanyakazi na biashara haramu ya binadamu.
Zaidi ya wanajeshi 3,000 wapya walianza mafunzo Jumatatu nchini DRC huku jeshi la nchi hiyo likiimarisha mapambano yake dhidi ya waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda. Serikali ya Rwanda, ambayo imekanusha mara kwa mara kuunga mkono kundi la M23, ilisema kuwa ndege ya kivita ya Congo "imekiuka anga ya Rwanda kwa kutua kwa muda katika uwanja wa ndege wa Rubavu. Baadaye Congo ilisema kwamba ndege hiyo iliyokuwa haina silaha ilitua kwa bahati mbaya katika anga ya Rwanda.