Chama cha The Greens cha shirikisho chataka swala la mkataba na jamii yawa Australia wakwanza, lijumuishwe kama sehemu yakutoa sauti yawa Australia wa kwanza bungeni.
Mamilioni ya Wakenya wameanza kumiminika katika vituo vya kupigia kura mapema leo kumchagua rais mpya, bunge na viongozi wengine. Kiti cha urais kinawaniwa na wagombea wanne ambao ni mwanasiasa mkongwe Raila Odinga, Makamu Rais William Ruto, George Wajackoyah na David Mwaure. Kura za maoni zimetabiri ushindani mkali kati ya Odinga na Ruto. Jumla ya wapiga kura milioni 22 wamejiandikisha kushiriki uchaguzi wa leo utakaohitimisha utawala wa rais Uhuru Kenyatta.
Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi anatarajiwa kujadili mvutano ulioko kati ya nchi yake na Rwanda wakati wa ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken mjini Kinshasa leo Jumanne, ofisi ya rais ilisema Jumatatu. Mvutano ulizuka tena kati ya DRC na jirani yake Rwanda, serikali ya DRC ikiishtumu Rwanda kuunga mkono waasi wa M23, tuhuma ambazo zinakanushwa na serikali ya Rwanda.