Wakaazi wamagorofa mjini Melbourne walio fungiwa ndani wakati wa kilele cha vizuizi vya UVIKO-19, kuchangia fidia ya $5 milioni ambayo serikali ya Victoria imekubali kutoa baada ya kesi dhidi yake kusikizwa mahakamani.
Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo inafanya maombolezo ya kitaifa kuwakumbuka zaidi ya watu 400 waliofariki mwishoni mwa juma kufuatia mafuriko. Mafuriko hayo yalisababishwa na mvua kubwa katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Kalehe jimboni Kivu Kusini.
Waziri mkuu wa zamani wa Burundi mwenye ushawishi mkubwa Alain Guillaume Bunyoni alifikishwa mahakamani Jumatatu akituhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa na kumkashifu rais, chanzo cha mahakama na mashahidi walisema. Bunyoni alikuwa waziri mkuu kuanzia katikati ya mwaka 2020 hadi Septemba 2022, lakini alifutwa kazi baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kuchukua hatamu za uongozi.
Jopo la majaji watano nchini Nigeria siku ya Jumatatu walikaa kikao cha kwanza kusikiliza kesi inayowahusisha viongozi wa upinzani walioshiriki uchaguzi wa mkuu wa rais wa mwezi Februari ambao chama tawala kilishinda. Tangu Nigeria irejee kwenye demokrasia mwaka 1999 miongo mitatu baada ya utawala wa kijeshi, uchaguzi umekuwa ukiishia mahakamani, ingawa hakuna pingamizi iliyowahi kutengua matokeo.