Moja ya mashirika maarufu yanayo toa msaad kwa wakimbizi kwa jina la Asylum Seeker Resource Centre, limesema limeko katika hatari yakufungwa. Shirika hilo limetoa taarifa kuwa misaada inayopokea imepungua kwa 45% tangu Julai mwaka jana. Shirika hilo hutoa ushauri wakisheria pamoja nakutoa msaada kwa watu wanao omba hifadhi. Shirika hilo limezindua ombi kwa umma kwa msaada wa haraka, likisisitiza kuwa shirika hilo lina hela zakutosha kutoa huduma kwa muda wa wiki sita tu.
Shirika la Waandishi wa Habari wasio na mipaka RSF limeukosoa mchakato wa kisheria kuhusu kifo cha mwandishi wa habari mashuhuri nchini Rwanda na ambaye alikuwa akiukosoa utawala wa Rais Paul Kagame. John Williams Ntwali, aliyekuwa mhariri wa gazeti la The Chronicles, alifariki Januari 18, gari lilipogonga pikipiki aliyokuwa akiendeshwa kama abiria karibu na mji mkuu wa Kigali.
Wanajeshi saba wa Congo wamehukumiwa kifo kwa kuonyesha 'uoga mbele ya adui' na kusababisha hofu kuu walipokimbia waasi wa M23. Siku ya Alhamisi, wanajeshi hao walipitia katikati ya Sake, kilomita 25 magharibi mwa mji mkuu wa mashariki mwa Kongo wa Goma, "wakipiga risasi kiholelea, walipokuwa wakiwakimbia adui kutoka mstari wa mbele", mwendesha mashtaka wa kijeshi alisema katika mahakama ikiendelea siku ya Jumamosi huko Sake. Wanajeshi hao walikanusha mashtaka na mawakili wao walisema watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama, mamlaka ya mkoa wa Kivu Kaskazini ilisema.