Baadhi ya wabunge katika vyama vya Liberal na Nationals, wanataka Bw McCormack ajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho ili amruhusu naibu wake David Littleproud, achukue uongozi wa chama hicho nakurejesha ustawi.
Waziri wa Afya nchini Rwanda Dkt. Diane Gashumba, amejiuzulu kulingana na afisi ya waziri mkuu nchini humo. Kujiuzulu kwake kunajiri wiki moja tu baada ya mawaziri wengine wawili kutangaza kujiuzulu. Evode Uwizeyima, ambaye alikuwa akisimamia maswala ya kisheria alikiri kumpiga mlinzi mmoja. Isaac Munyakazi alijiuzulu kama waziri anayesimamia elimu ya msingi na ile ya upili.
Uganda imewekwa katika hali ya tahadhari ya upungufu wa chakula wakati nzige kutoka jangwani wakiendelea kushambulia wilaya mbalimbali nchini humo.