Zaidi yawatu 266 walio hamishwa kutoka mjini Wuhan, wata ishi kwa muda wa wiki mbili wakiwa wametengwa katika kambi ambayo haija tumiwa katika eneo la kaskazini ya mji wa Darwin. Wakati baadhi ya wakazi wa Darwin hawajafurahia watu hao kupewa makazi karibu ya mji wao, wakazi wengine wamesema hawana wasi wasi wowote.
Umati wa wakazi wa Kenya Jumamosi asubuhi walijipanga kwenye mitaa ya Nairobi wakisubiri kuingia majengo ya Bunge la Kenya kuuaga mwili wa Raiswao wa zamani nchini humo, Daniel Toroitich Arap Moi alifariki Jumanne ya Februari 4 mwaka huu (2020) akiwa na umri wa miaka 95. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret Kenyatta walikuwa watu wa kwanza siku ya Jumamosi, kuuaga mwili wa Rais wa pili wa Kenya, Daniel Arap Moi kwenye majengo ya bunge katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Image
Rais Donald Trump amewafuta kazi maafisa wawili waandamizi waliotoa ushahidi dhidi yake katika kesi ya kutokuwa na imani naye iliyokuwa inamkabili. Balozi wa Marekani kwa Muungano wa Ulaya, Gordon Sondland, amesema "Nimeambiwa kwamba rais anataka nirudi nyumbani mara moja". Awali, Luteni kanali Alexander Vindman, mtaalamu mkuu katika masuala ya Ukraine, alisindikizwa kutoka nje ya Ikulu ya Marekani.