Serikali ya shirikisho yasema Australia iko katika sehemu imara, yakujibu janga la coronavirus baada ya barakoa na chanjo za mafua za ziada kuwasili nchini. Na wahudumu wa afya kwa maranyingine wamekumbushwa tena, wabaki nyumbani kama wana dalili zozote zaku umwa.
Viongozi wa nchi za Afrika, Benki kuu ya Dunia (WHO) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wametoa wito wa hatua ya dharura ya kimataifa kusaidia nchi za Afrika kukabiliana na janga la virusi vya corona.
Waziri wa fedha wa Ujerumani Olaf Scholz amesema katika mahojiano yaliyochapishwa leo Jumapili kuwa huenda nchi hiyo ikaweza kudhibiti athari za kibajeti kutokana na janga la virusi vya corona bila kuvuka viwango vya deni vilivyoidhinishwa iwapo uchumi utarejea katika hali ya kawaida katika nusu ya pili ya mwaka huu.