Wanasayansi na watafiti walijumuika mjini Melbourne katika kongamano la kwanza duniani kujadili swala la malaria. Ilikuwa fursa ya walio hudhuria kongamano hilo, kuchangia uzoefu wao pamoja naku jadili mbinu zaku tokomeza malaria.
Nancy Stephen Matowo ni mtafiti na mwanasayansi, katika taasisi ya afya ya Ifakara nchini Tanzania. Alishiriki katika kongamano hilo, ambako alichangia utafiti wake na wanasayansi na watafiti wenzake.
Bi Nancy ali eleza shirika la habari la SBS Swahili kuhusu utafiti wake nchini Tanzania, pamoja na hatua ambazo zina tekelezwa katika taifa hilo la Mashariki ya Afrika kulisaidia kutokomeza malaria.
Share






