Mara ya mwisho kongamano hilo lili andaliwa ilikuwa miaka mitatu iliyo pita, rais wa China Xi Jinping ali ahidi zaidi ya dola bilioni 60 za marekani kupitia mikopo na msaada kwa bara la Afrika.
Viongozi hao nama waziri wao, wanatarajia kupokea misaada mingine tena. Wakazi wa baadhi ya mataifa ya Afrika wame lalamika kuhusu, hatua zakutumia raia wa China katika ujenzi wa miradi, badala yakutoa ajira hizo kwa wenyeji, na kile kinacho dhaniwa kuwa ni mikataba maalum yamakampuni yawa China.
Kuna uwezekano wasi wasi huo utaongezeka, wakati mataifa katika sehemu zingine za dunia, hususan katika jimbo la kusini mashariki Asia, yana anza kuhoji kama msaada wa China unatolewa kwa gharama kubwa.
Kila taifa barani Afrika lili wakilishwa katika kongamano hilo la biashara isipokuwa taifa la eSwatini (ambalo zamani lili julikana kama Swaziland), taifa hilo ndilo mshiriki wa pekee wa jimbo la Taiwan barani Afrika, na kufikia sasa taifa hilo limekataa wito wa China, wakusitisha uhusiano wake na Taiwana nakutambua China badala yake.