Kiongozi mpya wa chama cha Greens ni Adam Bandt, na chama cha Nationals kina naibu kiongozi mpya ambaye ni David Littleproud.
Wakati huo huo chama cha upinzani cha shirikisho kimesema lengo la siku ya kwanza ya kikao cha bunge hii leo jumanne, inastahili kuwa kupotezwa kwa maisha, mali na wanyama katika janga la moto wa vichaka.