Serikali inahitaji kuwashawishi maseneta wa vyama vingine, kupitisha muswada wake kwa ukamilifu, kwa sababu chama cha Labor kina ongoza kampeni ya kugawa muswada huo.
Wiki ijayo, seneti ita endelea na mjadala kuhusu mpango unao salia wa makato ya kodi kwa biashara ambayo serikali imependekeza. Makato hayo yatapunguza kiwango cha kodi ya makampuni kutoka 30% hadi 25%.
Mnamo mwezi Aprili, serikali ilikosa kura mbili tu, kupitisha muswada huo, na tangu wakati huo , seneta wa chama cha One Nation Pauline Hanson, amebadili msimamo wake waku isaidia serikali kupitisha muswada huo.
Wakati huo huo Seneta Brian Burston, aliye timuliwa kutoka chama cha One Nation, kuhusu swala hilo, amejiunga na chama kipya chakisiasa cha Clive Palmer na amesema ata tekeleza makubaliano aliyo fanya na seneta Cormann, kuunga mkono makato hayo ya kodi kwa ukamilifu.