Tony Shihemi ni mjasiriamali ambaye biashara yake yakusaidia watu kufanya mazoezi ilikuwa nawateja wengi sana kabla ya mlipuko wa janga la UVIKO-19.
Baada ya mlipuko wa janga la UVIKO-19 pamoja na vizuizi vilivyo fuata kudhibiti usambaaji wa virusi hivyo, Bw Shihemi pamoja na wajasiriamali wenza walijipata katika hali ngumu iliyo walazimisha kufunga milango ya biashara zao kwa muda usiojulikana.
Je! Bw Shihemi yuko tayari kufungua milango ya biashara yake tena baada ya malengo ya utoaji wa chanjo jimboni humo kutimizwa? Bw Shihemi alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS kuhusu mipango yake yakuwapokea wateja tena, punde baada ya mamlaka husika kutoa idhini. Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.