Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump na mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton wameshiriki katika mdahalo wa pili kabla ya uchaguzi mkuu wa urais wa Novemba.
Wagombea hao wawili walikabiliana vikali katika mada kama ulipaji kodi, sera zakigeni na katika mikanda ya video iliyovujwa ambapo Trump alisikika akijivunia jinsi huwa anawadhalilisha wanawake.
Hali hiyo imesababisha baadhi ya vigogo wa Republican kuondoa uungaji mkono wao kwa Bw Trump katika ugombea wa Urais.
Wiki chache zinasalia kabla ya siku rasmi ya kura ya urais, je Donald Trump atajinusuru au kashfa zinazo mkabili zime zika matumaini yake?
Share

