New South Wales inapanga kutoa mpango wake baada ya chini ya 80% ya utoaji wa chanjo, wakati Victoria inajiandaa kuregeza baadhi ya vizuizi jimboni humo.
Ila kuna taarifa nzuri, kwa wakaaji wa kanda ya Victoria kama Geelong na Surf Coast wataondoka katika amri za kubaki ndani leo usiku saa tano dakika hamsini, licha yakuwepo kwa kesi chanya ya COVID katika jimbo la Geelong. Hata hivyo eneo la Mitchell Shire litasalia ndani ya amri yakubaki ndani, kwa sababu ya ongezeko ya kesi.
Hiyo imejiri wakati serikali ya Victoria imetoa taarifa ya majiribio yake ya chanjo za uchumi, yanayo fanyiwa katika kanda ya Victoria kuanzia tarehe 11 Oktoba ambayo ni mwezi ujao. Majaribio hayo yataruhusu sehemu zamatukio kuwa wenyeji kwa wateja wengi walio pata chanjo kamili, katika sehemu za mahoteli, vinyozi, utalii na burudani. Serikali bado haija weka wazi mbinu bora yakuthibitisha hali ya mtu binafsi aliyechanjwa ila, inatumai kuwa rekodi za chanjo zinaweza ungwa na app ya Services Victoria ili iweze toa thibitisho.