Serikali ya Kenya imetoa muda wa siku 14 kwa shirika la umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi UNHCR, kuzifunga kambi za wakimbizi za Daadab na Kakuma kufuatia vitisho vya kiusalama vinavyosababishwa na baadhi ya wakimbizi.
Hatua ya serikali ya Kenya kutoa muda huo wa wiki mbili kwa shirika la UNHCR kufunga kambi hizo za wakimbizi, imetafsiriwa kama iliyochochewa na mgogoro baina yake na Somalia.
Serikali ya Kenya na ya Somalia, zimekuwa katika mgogoro wa kidiplomasia baada ya Somalia kuishitumu Kenya kwa kuingilia maswala yake ya ndani.
Share






