Uchaguzi huo ambao mara ya kwanza uliratibiwa kufanywa mwaka wa 2016, uli ahirishwa mara kadhaa na sasa, sehemu za nchi hiyo zina kumbwa kwa vurugu pamoja na madai ya ufisadi.
D-R Congo haija wahi kuwa na ukabidhaji wa mamlaka tangu nchi hiyo ilipo pata uhuru toka kwa ubelgiji mnamo mwaka wa 1960. Machafuko mapya yame jiri wakati serikali ime amuru umoja ulaya, iondoe mjumbe wake nchini humo.
Hatua hiyo imejiri kulipiza kisasi, kwa vikwazo ambavyo muungano wa ulaya imewekea maafisa 14 wa serikali, ambao wanajumuisha waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa rais Kabila.