Kifo cha Rais Peter Nkurunziza kime iweka Burundi katika utata wakikatiba.
Alexis Yesashimwe ni mchambuzi wamaswala yakisiasa nakikatiba kutoka Burundi, yeye pia ni mtaalam wamaswala yamariadhiano. Bw Yesashimwe ni mwanabodi pia wa shirika la Resilience International.
Katika mazungumzo na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bw Yesashimwe aliweka wazi jinsi katiba ya nchi hiyo inavyo tabiriwa kwa swala kama hili, pamoja na hatua ambayo mahakama yakikatiba ya Burundi imechukua kumaliza sintofahamu ambayo kifo cha Rais Nkurunziza kime zua nchini humo.
Share





