Wadau wengi na mashabiki wa soka nchini Australia, walikuwa tayari wame anza kuhesabu siku zake katika wadhifa huo.
Gumzo lilikuwa limeanza tena baada ya wageni Wellington Phoenix, kuongoza mapema katika mechi yao dhidi ya wenyeji Wanderers katika uwanja wa wenyeji, mashabiki wakianza kuelekeza hasira zao kwa mwalimu na viongozi wengine wa timu.
Baadhi ya mashabiki wa timu hiyo, wali eleza Idha ya Kiswahiil ya SBS, hisia zao kuhusu mwalimu na timu yao pamoja na mechi walio shuhudia, ambako technolojia ili ingilia kati kusaidia timu hiyo kupata ushindi ambao ilihitaji na pengine kuokoa kazi ya mwalimu na wasaidizi wake.