Wagombea katika uchaguzi wa Victoria wana kamilisha kampeni zao, masaa machache kabla ya uchaguzi Jumamosi 24 Novemba 2018.
Ni masaa machache tu yanayo salia, kuwashawishi wapiga kura nani anastahili ongoza jimbo hilo kwa miaka minne ijayo.
Wagombea kutoka vyama vikubwa wanapigia debe pia, sera zao kwa wapiga kura kutoka jamii za tamaduni tofauti jimboni Victoria.
Chama cha Labor kwa sasa kina viti 46 kati ya viti 88 bungeni, wakati chama cha mseto kina viti 37, na chama cha Greens kina viti vitatu na wabunge huru wana viti viwili bungeni.
Share






