Badala yake, Bw Minns amesema serikali yake, inalenga suluhu za muda mrefu.
Katika ishara kwa jinsi janga la upangaji limekuwa nchini Australia, bei ya kodi ya kati kwa wiki kwa nyumba katika gorofa mjini Sydney kwa mara ya kwanza imepita $600.
Bei ya kati ya kodi katika miji mikuu yote nchini Australia, imeongezeka kwa 24% katika mwaka uliopita kulingana na ripoti ya kodi ya Domain kwa robo ya Machi [[2023]].
Data ya CoreLogic inaonesha kuwa bei ya kodi ya kila wiki imefika $699. Kanda ya Australia nayo pia imeshuhudia ongezeko kubwa la kodi. Katika miaka mitano iliyopita, kodi za kati zimeongezeka kwa 80% katika mji wa pwani wa Gladstone jimboni Queensland.