Wiki hii, tume ya uzalishaji ilitoa ripoti mbili muhimu kwa afya ya akili nakujiua, ripoti hiyo imetoa mapendekezo kwa jinsi yaku toa mageuzi ambayo yame elezewa kuwa, yanahitajika sana katika sekta hiyo.
Ripoti hiyo ili elezea mahitaji yakuwa na mageuzi ni muhimu zaidi, ukizingatia madhara ya janga kwa afya ya akili pamoja na, ukame unao endelea, na moto wa vichaka wa msimu wa majira ya joto uliopita ambao ulisababisha uharibifu mkubwa.
Imeongezea kuwa matukio haya yame waathiri wa Australia wengi sana, kama nikupitia hatua zakujitenga kijamii, kupoteza ajira, nyumba, kuyumba kifedha au vurugu ya nyumbani.