Hali inaendelea kuwa tata kwa viongozi wa upinzani nchini Tanzania, wengi wao wakijipata chini ya udhibiti wa vyombo vya usalama nchini humo.
Hatua hiyo imejiri baada ya viongozi hao kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu, yaliyo mpa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi John Magufuli ushindi.
Vingozi wa upinzani wamedai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki wala huru, na wanataka uchaguzi mpya uandaliwe. Viongozi hao pia wame wahamasisha wafuasi wao wajiunge nao katika maandamano dhidi ya matokeo hayo.
Bofya hapo juu usikie makala ambayo mwandishi wetu Jason Nyakundi ameandaa kwa hoja hii.
Share






