Nimuhimu kujua jibu hilo kwa sababu ungonjwa wa moyo, ni moja ya sababu kubwa ya vifo nchini Australia.
Utafiti uliofanywa na shirika ambalo huchunguza maswala ya moyo maarufu kwa jina la Heart Foundation mnamo mwaka wa 2017, ulipata kuwa mu Australia mmoja kati ya watatu hawajui dalili za kawaida za mshtuko wa moyo. Hivi ndivyo unaweza tambua dalili hizo.
Kwa taarifa ya ziada, tembelea tovuti ya shirila la Heart Foundation na Heart Support Australia.
Iwapo unahitaji msaada wa lugha, pigia simu huduma ya tafsiri na ukalimani kupitia namba hii 13 14 50, na omba shirika hilo ambalo ungependa zungumza nalo.
Piga simu kwa namba hii pia 000, iwapo wewe au mtu unaye mjua, anakabiliana na dalili za mshtuko wa moyo.