Ugonjwa huo sugu huathiri mu Australia mmoja kati ya watu kumi wenye umri wa miaka 65 na zaidi.
Wakati hakuna tiba yaku ponya ugonjwa huo, mtaalam wa lishe ya wazee ana amini unaweza danganya kupungua kwa uwezo wa ubongo kukumbuka na kufikiri, kwa kula vyakula bora kwa ubongo.
Huenda bado tuna safari ndefu yaku pata tiba ya ugonjwa wa kupungua kwa uwezo wa ubongo kukumbuka na kufikiri. Ila kwa sasa, unaweza jifunza mengi kuhusu jinsi yaku ongeza afya ya ubongo wako kwaku tembelea tovuti ya maswala ya ubongo wako. Iwapo unataka taarifa ya ziada kuhusu jinsi yaku mudu maisha ukiwa na ugonjwa wa kupungua kwa uwezo wa ubongo kukumbuka na kufikiri, unaweza pigia simu shirika la Alzheimer’s Australia kwa namba hii: 1800 100 500 au tembelea tovuti yao: fightdementia.org.au
Unaweza pigia simu pia shirika la National Dementia Helpline kwa msaada wa huduma yawa kalimani kwa namba hii: 131 450.