Tume ya uchunguzi kwa gereza za watoto katika wilaya ya kasakazini ime sikia ushahidi kuhusu jinsi mtoto mmoja alivyo nyimwa chakula na maji kama adhabu, pamoja nakulazimishwa kujisaidia ndaniya mto waku lalia.
Dylan Voller ni mfungwa wa zamani katika gereza la watoto la Don Dale ambalo liko mjini Darwin.
Dylan ni mmoja kati ya wafungwa kadhaa ambao, uchunguzi waki taifa ume anzishwa kuchunguza walivyo dhulumiwa gerezani.
Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 19 ni mmoja wa mashahidi muhimu, baada ya taarifa za habari zilizo onesha akiadhibiwa kwa gesi yakutoa machozi, pamoja nakufungwa katika kiti akiwa amefunikwa kichwa.
Share
