Miongoni mwa wapiga kura 48 walio kuwa ndani ya chumba cha mjadala huo na, ambao walikuwa hawaja amua watakaye mpigia kura, wengi wao walisema Bw Shorten ndiye aliyeshinda mjadala huo.
Kabla ya mjadala huo kuanza, tume ya uchaguzi ya Australia, ilitangaza kuwa idadi ya watu takriban laki moja elfu 10, tayari wamepiga kura zao mapema (29Aprili) katika siku ya kwanza yakupiga kura mapema katika uchaguzi wa shirikisho wa 2019.
Wale ambao hawaja piga kura mapema tayari, wata tazama mjadala wa pili wa viongozi hao ijumaa tarehe 5 Mei mjini Brisbane, kwenye runinga yakulipia, wakati Bw Morrison anataka mjadala wa tatu ufanywe tarehe nyingine baada ya mjadala huo na wakati kila mtu anatazamiwa kutazama runinga.