Ila wakati mioto ya mwisho ina endelea kuzimwa, waathiriwa wengi wana anza kuhisi changamoto zakiakili zinazo letwa na kazi ngumu iliyo mbele yao.
Shirika la huduma ya akili ya afya kwa jina la Lifeline, imeshuhudia ongezeko kubwa ya wito wa simu katika historia ya shirika hilo ambalo limetoa huduma kwa miaka 57.
Licha ya machungu hayo yote, pamekuwa afueni pia. Wasanii wenyeji walishirikiana na wasanii wakimataifa, katika tamasha maalum mjini Sydney ambako maelfu ya watu walihudhuria tamasha yakufanya mchango kwa waathiriwa wa moto huo wa vichaka. Takriban dola milioni 10, zilichangwa katika tamasha hiyo kuwasaidia wa Australia kuanza maisha nakujenga upya.