Ila wakati mpangilio huo unakaribia isha, waendesha magari wa Australia wanajiandaa kukabiliwa kwa bei za juu za petroli.
Kwa miezi mitano iliyopita, gharama ya petroli nchini Australia ilipungua kwa sababu yamakato kwa kodi ya mafuta. Makato hayo yalitekelezwa na serikali yazamani, serikali hiyo ilikata kiwango cha kawaida cha kodi ya senti 44.2 kwa lita hadi senti 22.1 kwa lita.
Ila makato hayo yalikuwa yameratibiwa kudumu hadi 28 Septemba, na serikali mpya ya shirikisho imesema haita badili hali hiyo.