Wakati huo huo serikali ya jimbo hilo ina inua kikomo cha malipo ya mwaka huu baada ya miezi ya hatua za viwanda.
Kiongozi wa jimbo hilo ametangaza pia uwekezaji wa bilioni 4.5 za dola, kwa mfumo wa afya ambao unakabiliwa na matatizo, sehemu ya msaada unao tolewa unajumuisha mpango waku waajiri wafanyakazi wa matibabu elfu kumi, pamoja na kutoa dola elfu tatu za ziada kwa wafanyakazi walioko katika mfumo wa afya kwa saa.
Serikali ya jimbo ina inua pia kikomo cha malipo kwa sekta ya umma, ambayo imekuwa ikitumia tangu 2011. Malipo yanatarajiwa kuongezeka kutoka 2.5% hadi 3% katika mwaka huu wa fedha. Malipo hayo yataongezeka tena hadi 3.5% mwaka ujao yakitegemea uzalishaji wa waajiriwa. Hiyo ni hatua inayo wathiri wafanyakazi laki nne wa serikali jimboni wanao jumuisha wafanyakazi wa afya, walimu, maafisa wa jeshi la polisi na wanao fanya kazi za usafi.