Bi Amina ni mkaaji wa kitongoji cha Goodna, siku chache zilizo pita hali mbaya ya hewa na ongezeko ya mafuriko, yali mlazimisha yeye na familia yake kuhama nyumba yao ghafla nakukimbilia kwa familia yao inayo ishi mbali kidogo ya eneo hilo la mafuriko.
Bw Blaise ni mkaaji wa Logan ambaye kwa mara nyingine amejipata katika hali tata kwa sababu ya mafuriko ambayo yamezingira kitongoji chake, nakufanya wakaaji wote wa eneo anako ishi kuwa kama wafungwa kwa sababu hakuna namna yakuingia au kuondoka katika eneo hilo kwa sababu ya wingi wa maji.
Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, wahanga hao wawili walitueleza masaibu wanayo kabiliana nayo, na jinsi wamejinusuru pamoja na hatua zingine wanazo endelea kuchukua kujinusuru kutoka janga hilo. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.