Ila mwaka huu wadau wengi wame ipongeza tume ya uchaguzi ya Kenya, kwa jinsi ilivyo simamia uchaguzi mkuu licha ya matatizo kadhaa kuibuka.
Tume hiyo imepongezwa haswa kwa kuchapisha matokeo ya chaguzi kadhaa kwenye tovuti yake, ambako mtu yeyote ana uhuru waku yapakua naku yajumlisha kwa raha zake.
Bw George ni mfuasi wa mrengo wa Kenya Kwanza anaye ishi Australia, katika mahojiano maalum kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya aliweka wazi tofauti ya uchaguzi huu na uchaguzi mkuu wa 2017 ulio batilishwa na mahakama kuu ya Kenya. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.